Proverbs 7:10-27


10 aNdipo huyo mwanamke akatoka kumlaki,
hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu.
11 b(Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi,
miguu yake haitulii nyumbani;
12 cmara kwenye barabara za mji,
mara kwenye viwanja vikubwa,
kwenye kila pembe huvizia.)
13 dHuyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu,
na kwa uso usio na haya akamwambia:

14 e“Nina sadaka za amani nyumbani;
leo nimetimiza nadhiri zangu.
15Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki;
nimekutafuta na nimekupata!
16 fNimetandika kitanda changu
kwa kitani za rangi kutoka Misri.
17 gNimetia manukato kitanda changu
kwa manemane, udi na mdalasini.
18 hNjoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi;
tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!
19Mume wangu hayupo nyumbani;
amekwenda safari ya mbali.
20Amechukua mkoba uliojazwa fedha
na hatakuwepo nyumbani karibuni.”

21 iKwa maneno laini yule mwanamke akampotosha;
alimshawishi kwa maneno yake laini.
22 jMara huyo kijana alimfuata yule mwanamke
kama fahali aendaye machinjoni,
kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,
23 kmpaka mshale umchome ini lake,
kama ndege anayenaswa kwenye mtego,
bila kujua itamgharimu maisha yake.

24 lSasa basi wanangu, nisikilizeni;
sikilizeni kwa makini nisemalo.
25 mUsiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke,
wala usitangetange katika mapito yake.
26 nAliowaangusha ni wengi;
aliowachinja ni kundi kubwa.
27 oNyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini,
Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.
Copyright information for SwhNEN